Huu Hapa Ndio Uchawi Anaoutumia Diamond Platnumz ili Kupata Mafanikio - Mapenz Wakubwa

Hot

Thursday, October 28, 2021

Huu Hapa Ndio Uchawi Anaoutumia Diamond Platnumz ili Kupata Mafanikio


Watanzania wengi hawaamini mafanikio yanaweza kuja bila Uchawi, mara nyingi mtu akizungumzia mafanikio ya Diamond Kimuziki, Uchumi, kijamii, nakadharika, basi utasikiaa "aah yule ni Freemason, anatumia sana uchawi yule''

Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya Diamond hayatokani na nguvu yoyote ya giza bali ni Jitihada zake mwenyewe. Kama Diamond kafanikiwa kupitia Uchawi, wasanii wangapi Tunapishana nao kwa waganga ila maisha yao hayabadiliki Daima na milele.


Uchawi wa Diamond ambao umefanya mpaka sasa amefanikiwa na anaendelea kufanikiwa zaidi ni:

-Kufanya kazi kwa Bidii.
-Nidhamu.
-Ujanja mwingi wenye Faida.
-Bingwa wa kutafuta Connection.
-Bingwa wa kutengeza attention na nchi nzima ikamzungumia yeye.
-Anajua Mashabiki zake wanataka nini, na kwa muda gani.
-Hariziki na alichonacho.
-Haogopi kuiga jambo Zuri na yeye kuongezea ubunifu wake.
-Anaamini katika Team Work.
-Anajua Biashara ya muziki.
-Anajua kulitumia vyema jina lake (Brand)
-Anauwezo wa Kubrand Wasanii wake na Wakamuingizia Faida Badae.
-Anapokea mawazo Mapya.
-Anajua Kutafuta pesa nje ya Muziki.
-Anajua alipotoka, hivyo hana mchezo kabisa katika masuala ya Kutafuta hela.


WASANII HAMNA BUDI KUPITA NJIA ANAZOPITA HUYU MWAMBA, KUMCHUKIA, KUMPONDEA, HAKUTA WASAIDIA KITU, KWENYE MAZURI SIFIENI.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3EnVe7c
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/3bl3RTA

No comments:

Post a Comment