Mapenz Wakubwa: Mapenzi

Hot

Showing posts with label Mapenzi. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi. Show all posts

Friday, January 26, 2024

Watoto wa Manara, Baba Levo watoboa matokeo Kidato cha Nne

January 26, 2024 0

 

Watoto wa Manara, Baba Levo watoboa matokeo Kidato cha Nne

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2023, yakionyesha kuongezeka kwa ufaulu wa watahiniwa kwa asilimia 0.87 na ufaulu wa hisabati ukipanda kuliko masomo yote.


Mbali na kuongeza kwa kiwango cha ufaulu, ubora wa ufaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu nacho kimeongezeka kwa asilimia 0.47 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2022.


Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema asilimia 37.42 ya watahiniwa wamepata daraja la kwanza hadi la tatu ikilinganishwa na asilimia 36.95 waliopata madaraja hayo mwaka 2022.


“Jumla ya watahiniwa wa shule 471,427 kati ya 527,576 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 89.36 wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza hadi la nne.


Waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ni asilimia 37.42,” amesema Dk Mohamed. Kwenye matokeo hayo wapo watoto wa watu maarufu akiwemo Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye kupitia mtandao wa Instagram ameandika;


"Well done My Young Boy Prince Hassan Haji, umeendelea kuipa heshma familia yetu na umenipa furaha sana Mwanangu, Ufaulu wako wa kidato cha nne umenipa mood nzuri,"


"Jana ilikuwa Siku nzuri sana kwangu,Nimemuoa Kipenzi changu Zaiylissa Buga, binti yangu Sayyidat Fatmah ilikuwa birthday na kidume kaniletea Division One ya ukweli,"


"Hongera Prince ila utambue ndio kwanza unaenda advance level (kidato cha tano na sita), safari yako ya kuisaka elimu ndio inaanza, nnalokuahidi ntakusomesha kwa kadri ntavyojaaliwa na nipo tayari kwa ajili yako ili utimize ndoto zako,"


Msanii wa Bongo Fleva, maarufu kama Baba Levo, amefurahishwa na matokeo ya kijana wake Levo, aliyepata one ya 13 kidato cha nne, akisifia kijana wake kafuata akili yake.


Kupitia mtandao wa kijamii Instagram, ameandika; "Hongera sana mwanangu Levo kwa kupata one ya 13 form four, umefata akili za mimi baba yako kabisa," mwisho wa kunukuu ambaye aliwahi kutamba na wimbo wake wa Ngongingo.


Kupitia mtandao huo wa Instagram, Dayna Nyange ameandika; "Ahsante sana mwanangu Rahma kwa ufaulu mzuri hakika mungu yu pamoja nasi, Dk Nyange mtarajiwa kabisaaa yaani leo I’m so so happy (nina furaha sana) and so proud of you my precious daughter Mungu akazidi kukutendea InshaAllah tukatimize malengo yetu, umenipa division one Kama ulivyo promise (ahidi) nakushukuru mama."



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/0x7cI5R
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/EPORdpu
Read More

Mwakinyo: Mpinzani Wangu Asipotokea Nitazichapa na Promota

January 26, 2024 0
Mwakinyo: Mpinzani Wangu Asipotokea Nitazichapa na Promota


Bondia namba moja Tanzania, amewatoa shaka mashabiki wa ngumi kuwa pambano lake litapigwa na kuahidi kuwaonyesha uwezo na kutoa burudani.


Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Mbiya Kanku wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika pambano la mtata mtatuzi litakalopigwa Januari 27, 2024 katika Uwanja wa ndani wa New Amaan Visiwani Zanzibar.


Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa huenda pambano hilo lililopewa jina la 'Mtata Mtatuzi' likavunjika tena, kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa na nia mbaya humtumia ujumbe mpinzani wake wakimtaka asipigane ili pambano hilo livunjike.


Akizungumza na Wanahabari leo Januari 25,2024 bandarini Jijini Dar es Salaam wakati akijiandaa na safari visiwa vya Karafuu (ZANZIBAR) Mwakinyo amesema amejipanga kuonesha mchezo ambao wengi hawajahi kuuona huku, akiahidi kutoa burudani kwa mashabiki wake.


“Mpaka sasa kila kitu kipo katika ubora kuelekea pambano langu. Lakini kuna changamoto kidogo kwa upande wa promota na kwangu pia inani confuse lakini sioni kama ni taarifa mbaya kwangu kwa sababu mashabiki zangu wana hamu wanione nikipigana, kwa hiyo mwisho wa siku lazima nipigane.


“Kuna maneno ya kwamba wapo baadhi ya watu wanamtumia meseji mpinzani wangu ili asitokee kwenye pambano ili liahirishwe na nionekane kwamba ni kawaida yangu kuharibu mapambano.


“Lakini ambacho tumekubaliana na promota (Meja Selemani Semunyu) ni kwamba iwapo kitatokea kitu kama hicho basi tutacheza mimi na yeye ilimradi mashabiki zangu wafurahi.


“Wengi wanaotamani wanione nikipigana ni wale wapenda maendeleo na wapenda ngumi, lakini kuna vikundi vya watu wachache wapinga maendeleo wenye roho mbaya nadhani ndiyo wanataka hivyo. Wanawaza nguvu yangu itakuwa wapi baada ya mimi kushinda pambano hilo, ndiyo maana wanakosa usingizi.


“Mimi ni kijana ninayepambania ndoto zangu, nimejiandaa vizuri ndani ya pambano nan je ya pambano, niko vizuri kote kote, kila kitakachotokea nimejiandaa kukabiliana nacho,” amesema Mwakinyo.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/t1UzgRa
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/B2pAs17
Read More

Kocha Benchikha wa Simba Kwenda Timu ya Taifa ya Algeria

January 26, 2024 0



Kocha wa Simba SC Abdelhak Benchikha ni moja ya makocha wanaopewa nafasi ya kwenda kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Algeria.

Kocha huyo raia wa Algeria anapewa nafasi hiyo baada ya Tetesi zinazoeleza kuwa Kocha Mkuu wa Algeria Djamal Belmad anataka kujiweka kando na timu hiyo.

Benchikha anatajwa kutokana na mafanikio aliyoyapata akiwa na USM Alger mwaka jana Kwa kutwaa Kombe la Shirikisho na CAF Super Cup.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/afCmXdh
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/5uYs2ad
Read More

Kocha Afcon amng'oa Bacca Yanga

January 26, 2024 0



MAKOCHA wawili mahiri waliowahi kuifundisha Yanga wameshtushwa na kiwango cha beki wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Ibrahim Bacca kwenye michuano ya Afcon. Na wameshangaa kuona kwanini bado anacheza ligi ya ndani.

Kocha Mbelgiji anayeinoa Gambia kwenye Afcon, Tom Saintfiet katika wachezaji wote wa Stars amemuelewa zaidi Bacca kwenye eneo la ulinzi na kutabiri kwamba muda wowote staa huyo atapata ofa Ulaya kwa vile ameonyesha utofauti mkubwa licha ya matokeo ya timu.

Saintfiet ambaye aliinoa Yanga mwaka 2012 kwa muda mfupi, alisema Bacca ni beki anayecheza jihadi wakati wote wa mchezo na kwamba kiwango chake kinastahili awe anajiunga na Stars akitokea klabu kubwa Ulaya au nje ya Afrika.

Saintfiet ambaye jana usiku timu yake ilikuwa inacheza na Cameroon kukamilisha ratiba kwenye Afcon, amekumbusha kiwango cha beki wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lakini akakiri mkongwe huyo amezidiwa na Bacca.

“Nilikuwa nahesabu wachezaji ambao wanatoka nje ya Tanzania, nilipofika kwa yule mwenye jezi namba nne nilishangaa kuona anacheza Yanga, naiheshimu Yanga ni klabu kubwa Tanzania na timu yangu ya zamani lakini huyu beki anatakiwa kucheza nje ya Tanzania hata Ulaya,” alisema Saintfiet.

“Ana tachi nzuri ya mpira lakini muda wote akili yake iko uwanjani kuzuia. Angalia anavyoteleza kuzuia mipira ni beki wa kisasa kabisa ambaye klabu nyingi zingependa kuwa naye,” aliongeza kocha huyo ambaye kabla ya jana usiku timu yake ilikuwa haina pointi hata moja.

Wakati Saintfiet akiyasema hayo kocha Mzambia George Lwandamina ambaye kwa sasa anainoa Zesco, alisema Bacca kucheza na Yanga ni suala la bahati kubwa kwa klabu hiyo.

Lwandamina alisema beki huyo kama angesimama na mshambuliaji Patson Daka aliyeisawazishia Zambia bao asingefunga kirahisi.

“Ni beki ambaye mshambuliaji yoyote hawezi kuwa huru kufanya kazi kwa akili yake, makocha wengi wanapenda kufanya kazi na mabeki wa aina hii, ni bahati sana kwamba bado yupo hapo Yanga lakini alitakiwa kuwa Ulaya.

“Nimemuangalia anatumia miguu yote vizuri hiyo ni faida kubwa kwa beki wa kati hasa anapokuwa mzuri kuruka na kutumia miguu yote inamfanya kuwa tayari kutoa msaada kwa pande zote za pembeni,” alisema Lwandamina ambaye aliikochi Yanga kuanzia 2016-2018.

Huu ni msimu wa pili kwa Bacca Yanga ambaye alijiunga na Yanga akitokea KMKM ya Zanzibar. Mchezaji huyo amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha Taifa Stars licha ya kwamba imekuwa na matokeo ya kusuasua baada ya kupoteza dhidi ya Morocco na kutoa sare na Zambia.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/8a10LCf
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/RI9z7GP
Read More

Thursday, January 25, 2024

AFCON : Hizi Hapa Nchi Zilizoingia 16 Bora Michuano ya AFCON

January 25, 2024 0


#AFCON2023 Na hawa ndiyo 16 Bora wa fainali hizi!!

Je, kuna ambaye hakustahili!!?

27/01/2024
Angola vs Namibia
Nigeria vs Cameroon,

28/01/2024
Guinea ya Ikweta vs Guinea,
Misri vs Congo DR

29/01/2024
Cape Verde vs Mauritania,
Senegal vs Ivory Coast

30/01/2024
Mali vs Burkina Faso
Morocco vs Afrika Kusini



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/51sKWbO
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/2oqWaIe
Read More

Wednesday, January 24, 2024

Etoo Awachana Wachezaji wa Cameroon 'Wachezaji Waliozaliwa Ulaya Hawana Uzalendo'

January 24, 2024 0

 

Etoo Awachana Wachezaji wa Cameroon 'Wachezaji Waliozaliwa Ulaya Hawana Uzalendo'

Samuel Eto'o amewachana wachezaji wa Cameroon waliozaliwa ulaya;


Wadogo zangu wapendwa naelewa, wengi miongoni mwenu hamjazaliwa Cameroon wala hamjawahi kucheza vilabu vya Cameroon. Nyie mlizaliwa ulaya huko mna haki juu ya viongozi.



Mimi Cameroon ilinifundisha kwamba, napokuwa na timu ya taifa natakiwa kuwa mwanajeshi. Niwe tayari kukikabili kifo napopambania bendera.


Leo Cameroon inapitia fedhea sababu wachezaji wengi hawana upendo wa asilimia  kwa taifa hili. Niwieni radhi kwa kujiongelea mimi kama mfano.


Kwaajili ya upendo nilionao kwa nchi yangu, nilikuwa na uwezo wa kucheza mechi mbili kwa siku moja. Niliwahi kufanya hivyo, "Roger Milla" aliwahi kufanya hivyo, pia hata "François Omam Biyick."


Unafikiri Cameroon ilikuwa ikitulipa zaidi ya vilabu tulivyokuwa tukichezea?! Hapana. Kuichezea Cameroon tulikuwa hatupati hata 1/10 ya kile tunacholipwa sehemu nyingine.


Kufa ukiipambania nchi yako, thamani yake inazidi pesa yoyote katika ulimwengu.


"Manga Onguene" alivunjika mguu akiipigania jezi ya Cameroon. Huyu alikuwa mtu hatari wakati wake, alikuwa mchezaji bora kuliko mimi. Licha ya kuvunjika mguu na kutelekezwa lakini bado aliendelea kuipa heshima nchi yetu.


Kitu nachokiona, tulifanya makosa kuwakabidhi bendera watu waliozaliwa nje ya Cameroon. Uzalendo kwa taifa upo mbali na hisia za mioyo yao. Hawana DNA na udongo wa Cameroon. Lakini baada ya Afcon kila kitu kitabadilika.


Tutahakikisha tunafanya kipimo cha uzalendo kwa kila kijana kabla ya kumvalisha jezi ya nchi yetu."



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/HqNvneJ
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/gEsWtBd
Read More

Young Africans kucheza mbili za kirafiki

January 24, 2024 0

 

Young Africans kucheza mbili za kirafiki

Uongozi wa Klabu ya Young Africans umesema umeanza mchakato wa kutafuta timu za nje kwa ajili ya mechi za kirafiki itakayokiweka sawa kikosi chao katika kipindi hiki cha maandalizi kabla ya kuanza kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mwishoni mwa juma lililopita Kocha Mkuu wa miamba hiyo ya soka nhini, Miguel Gamondi aliuomba uongozi wa timu hiyo kumtafutia mechi mbili za kirafiki na timu za nje ya Tanzania ili kujui uimara wa kikosi chake kabla ya mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mbali na hilo pia Gamondi anataka kuitumia michezo hiyo kuwatambulisha rasmi wachezaji wao wawili wa kimataifa waliowasajili kwenye dirisha dogo la msimu huu ambao ni Augustine Okrah na Joseph Guede.


Makamu wa Rais wa Young Africans hiyo, Arafat Haji amesema wameanza kutafuta timu hizo na anaamini mchakato huo hautachukua muda kukamilika sababu wana maelewano mazuri na timu nyingi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.


“Lengo letu ni kupata timu imara ambazo zitakipa kikosi chetu mazoezi mazuri kulingana na mashindano tunayoshiriki, ndio maana nikasema mchakato wa kuzisaka timu hizo umeanza na dhamira yetu ni kucheza mechi hizo tukiwa ugenini,” amesema Arafat.


Kiongozi huyo amesema malengo ya Young Africans msimu huu ni kufanya vizuri kwenye mashindano yote, hivyo kama viongozi wa juu wanapambana kuhakikisha wanampatia kocha wao kile alichokihitaji ili kumjengea urahisi wa kufanikisha kile ambacho wamekikusudia.


Kikosi cha Young Africans kimerejea kambini Avic Town wiki mbili zilizopita kujiandaa na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu na Kombe la FA huku timu hiyo ikiwakOsa baadhi ya nyota wake waliopo kwenye timu zao za taifa zinazoshiriki Afcon 2023.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/n7jfqZg
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/CvHsILo
Read More

Makonda afichua siri Mbowe kwenda Ikulu alipotoka gerezani

January 24, 2024 0



Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Paul Makonda ameeleza kuwa, kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwenda Ikulu alipotoka gerezani kilikuwa na maana halisi ya dhamira ya kukuza demokrasia ya Rais Samia Hassan.

"Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia anafanya kazi kwa msaada mkubwa we Mwenyezi Mungu katika kuongoza Taifa hili na ukitaka kujua hilo dalili mojawapo ya mtu anayeaaidia ni Mungu ni kuwa na Upatanishi"

"Rais Samia alianza kuwapatanisha Watanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao, kabilabwala kipato na kila aliyepeleka malalamiko alimsikiliza na kuchukua hatua"

"Mbunge wenu wa zamani hapa Hai hata sura yake imebadilika sababu ndani yake anajua Rais Samia ametumwa na Mungu na nanjua wengine watakebehi na kutoa tafsiri nyingi lakini jiulizeni swali moja...anayepanga ratiba za binadamu ni nani? Maana yake Mungu alishampanga Samia kuwa Rais"

"Mbowe katika mahabusu stendi yake ya kwanza kafikia Ikulu na alipotoka alieleza na kukiri kuwa dhamira ya maridhiano Dkt. Samia ni dhamira njema...halafu mtu huyohuyo anakuja tena kusema hakuna maridhiano na bado anapiga simu kwa Rais Samia kuomba michango na anapewa."




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/VjxOktF
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/si9lG5Q
Read More

Tuesday, January 23, 2024

Ivory Coast Star Breaks Down in Tears on Bench After Humiliating 4-0 AFCON Defeat

January 23, 2024 0



A 4-0 humiliation at the hands of Equatorial Guinea proved to be too much for one Ivory Coast player, who was seen crying on the bench after missing a chance to equalise
Ivory Coast's midfielder #8 Franck Kessie consoles Ivory Coast's forward #14 Oumar Diakite after Equatorial Guinea won the Africa Cup of Nations (CAN) 2024 group A football match between Equatorial Guinea and Ivory Coast at the Alassane Ouattara Olympic Stadium in Ebimpe, Abidjan on January 22, 2024
AFCON hosts Ivory Coast are now sweating on their knockout stage progression
Ivory Coast star Christian Kouame broke down in tears as their Africa Cup of Nations hopes were left hanging in the balance.


The tournament hosts suffered a shock 4-0 defeat at the hands of Equatorial Guinea, who are 39 places below them in the FIFA rankings. It meant they've finished third in their group, with their opponents securing top spot ahead of Nigeria.

Those two are both through to the knockout stages, but the Ivory Coast now face a nervy wait to see if the qualify as one of the four best-ranked third-placed teams across the six groups. It all proved to be too much for Kouame.


After being subbed off in the second half, the Fiorentina winger, 26, was seen crying on the bench as the second, third and fourth goals went in. He'd missed a golden chance to equalise before being replaced.

The weight of that error clearly weighed heavy on his shoulders as he watched on helpless from the sidelines. Come the full-time whistle, he wasn't the only one who cut an emotional figure.

The defeated Ivory Coast team were consoling each other having failed to live up to the expectations of them as one of the favourites to repeat their 2015 triumph.

Christian Kouame crying on the bench
Winger Christian Kouame could be seen crying on the bench during the 4-0 loss

They'll now have to wait until the completion of the group stage on Wednesday (January 24) to learn their fate, having won just one of their three games - a 2-0 victory over basement side Guinea Bissau in the opening fixture of the tournament.

That victory puts makes them better off than any of the other current third-placed teams. But the standings could change significantly in the next 48 hours.

In the other fixture in Group A, Nigeria beat Bissau 1-0. Egypt, meanwhile, are likely to be without Mohamed Salah should they progress after his agent estimated a three to four week recovery on his hamstring injury.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/6HBjqYX
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/SVHewTC
Read More

Monday, January 22, 2024

Simba Yafichua Bilioni za Mo Dewji

January 22, 2024 0



Simba imefichua kuwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'MO' alichangia Sh2.4 bilioni katika bajeti klabu hiyo kwa msimu wa 2022/2023.

Akitoa taarifa ya fedha ya klabu hiyo ya 2022/2023, Mhasibu wa Simba, Suleiman Kahumbu amesema awali walipanga kukusanya Sh12.3 bilioni kwa msimu huo na mchango wa MO ulichangia kwa kiasi kikubwa wakavula lengo hadi Sh15 bilioni.

“Katika bajeti ya fedha ya msimu wa 2022/23 rais wa heshima wa Simba Mohamed Deji alituchangia kiasi cha Sh2.4 bilioni, fedha ambazo zilienda moja kwa moja kwenye kufanikisha kukusanya bilioni 15 ambazo zimetupa faida kwa kiasi kikubwa," amesema Kahumbu.

Kahumbu amesema hayo Leo januari 21, 2024 katika mkutano wa mwaka wa klabu hiyo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/0wHxcug
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/elBpoDv
Read More

AFCON: Tanzania, Zambia share the spoils

January 22, 2024 0


San Pedro, Ivory Coast Tanzania national soccer team, Taifa Stars were  forced to a 1-1 draw by their neighbors, Zambia’s Chipolopolo.

have missed the chance to go second in group F of the Africa Cup of Nations (AFCON) after a 1-1 draw against a 10-man Zambia.

In the Group F match of AFCON 2023 played at Stade de San Pedro in Ivory Coast on Sunday night has seen both sides cherishing one point a piece.

Simon Msuva put the country’s envoys upfront in the 11th minute after being set up by his skipper Mbwana Samatta.

It was a nice move initiated by veteran midfielder Himid Mao who robbed of the ball from Zambian.

Just before halftime, Zambia captain Rodereck Kabwe was shown a second yellow card forcing referee to give him a marching orders after fouling Mbwana Samatta in an aerial combat.

In the second half, the Chipolopolo lads kept heads up by diffusing well each danger imposed by Stars.

In the 88th minute, their venom striker Patson Daka used well the corner-kick delivered by substitute Clatous Chama to balance the equation.


His towering header was simply too hot for Stars goalie Aishi Manula to punch it to safety.

As it stands, Tanzania continue to wait for their first win in AFCON and they were too close to seal it tonight.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/j3YUl6x
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/TnhXLIZ
Read More

AFCON : Tanzania yapokwa ‘tonge mdomoni’ na Zambia

January 22, 2024 0



Bao la dakika ya 88 la Zambia limefuta matumaini ya Tanzania kuandikisha ushindi wa kwanza katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (Afcon).

Tanzania iliandikisha goli la kwanza katika dakika ya 11 kupitia winga wake wa kimataifa Simon Msuva akiunganisha pasi maridhawa kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta.

Zambia ilipata pigo kwa kutolewa kwa kadi nyekundu kwa nahodha wao Rodrick Kabwe katika dakika ya 44.

Tanzania iliendelea kuutawala mchezo huo na kukosa nafasi kadhaa za wazi kuongeza goli la pili wakati Zambia ikicheza mchezo wa kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Mashambulizi hayo ya kushtukiza yalizaa matunda katika dakika ya 88 ambapo mshambuliaji wa klabu ya Leicester City ya England Patson Daka alipofunga bao la kusawazisha kwa kichwa kikali akiunganisha krosi ya Clatous Chota Chama anayechezea klabu ya Simba ya Tanzania.

Hii ni sare ya pili kwa Tanzania katika michuano ya AFCON. Sare ya kwanza waliipata kwa Ivory Coast katika michuano ya mwaka 1980 ambapo magoli yalikuwa 1-1. Katika michuano ya mwaka 2019 Tanzania ilipoteza michezo yote mitatu.

Kwa matokeo hayo sasa Tanzania inaendelea kushikilia mkia wa kundi Fwakiwa na alama moja huku Zambia na DRC wakiwa na alama mbili kila mmoja na kinara wa kundi ni Morocco wenye alama nne. Morocco na DRC walitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa awali wa kundi hilo.

Tanzania sasa itaminyana na DRC siku ya Jumatano katika mchezo wa mwisho wa makundi, Morocco na Zambia pia wataminyana siku hiyo. Mpaka sasa hakuna timu yoyote katika kundi hilo ambayo imekata tiketi ya kucheza katika hatua ifuatayo.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/5Kai9Jo
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/MANQvyd
Read More

Sunday, January 21, 2024

Ugonjwa wa Red Eyes Waikumba Familia Nzima ya Rapper Rosa Ree, Aweka Video Hii

January 21, 2024 0

 

Ugonjwa wa Red Eyes Waikumba Familia Nzima ya Rapper Rosa Ree, Aweka Video Hii

Ugonjwa wa Red Eyes waikumba familia nzima ya Rapper Rosa Ree, Aweka Video Hii

VIDEO:



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/vwMIuBz
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/z1HlXRV
Read More

Mange Kimambi: Kwenye Hii Kesi Dullah Kashinda, Kajua Kuwatoa Kwenye Reli Haji Manara na Zaylisa

January 21, 2024 0


Ameandika Mange Kimambi:

Mı sio mtu wa kupenda penda umbea wa mitandaoni au mtu wa kufatilia mambo ya watu ila ngoja tu niseme kitu, kwenye hii kesi Dullah kashinda aiseee, kajua kuwatoa kwenye reli sasa hivi kiki yoote yake insta….. Yani kajua kutembea na kiki ya watu….DAH!! Dadekiii.

Alafu hiyo sehemu Dulla aliyoimba kwamba Siri yetu niliificha eti ni kwamba Zay alimpa kisamvu cha kopo… eti ndo maana akalia machozi alikuwa analilia aendelee kupewa kisamvu cha kopo….. Sio maneno yangu!!!

So nyie mnaemcheka Dulla kulia vile mjiulize je ingekuwa wewe ndo umepewa kisamvu cha kopo alafu ghafla umekatizwa usingelia kama mbuzi jike?

Hawa jamaa tuwaache tu wamalizane wenyewe maana hawana tofauti kabisaaa, mmoja akiachwa analia mwingine akiachwa anazimia chini puuh!


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ROXDgrK
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/gcvy7rL
Read More

Saturday, January 20, 2024

Tutawapima Wabunge, Madiwani kwa Kazi na sio Maneno - Paul Makonda

January 20, 2024 0

 

Tutawapima Wabunge, Madiwani kwa Kazi na sio Maneno - Paul Makonda

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, leo Januari 19,2024 ameanza ziara yake kwa kuongea na Wakazi wa Tegeta Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema Wabunge, Wawakilishi na Madiwani watapimwa kwa kazi wanazofanya na sio kwa maneno au kujipendekeza kwa Viongozi ambapo amesemaa wasiofanya kazi taarifa zao zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM (Rais Dkt. Samia), kwamba hawafai kupewa nafasi ya kugombea tena mwaka 2025.


Makonda amenukuliwa akisema;


“Duniani kote hawajawahi kumaliza matatizo hata Mataifa makubwa tunayokimbilia kuyaomba bado yana changamoto, nilikuwa namsikia Rais wa Marekani anajadili jinsi gani wanataka kujenga barabara na madaraja kwenye Nchi yao Marekani nao wapo kwenye ujenzi wa barabara, tafsiri yake ni kwamba changamoto haziwezi ktuisha siku moja, zinaendelea kuwepo kutokana na idadi ya watu, mabadiliko ya tabianchi na hali ya kiuchumi, vinginevyo tungeweza kujenga lami kote”


“Mwaka huu 2024 na 2025 tutawapima Wabunge na Wawakilishi na Madiwani namna gani wanatatua changamoto za Wananchi wao na jinsi gani wapo mstari wa mbele kukijenga Chama chao, awamu hii CCM hii ya Dkt. Samia na Mimi nikiwa Msemaji na nimeshasema tangu nakabidhiwa ofisi sitobeba mzigo kila Mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kama hamfanyi kazi ya utekelezaji wa Ilani na kutatua changamoto za Watu, kwa kauli moja tutakupima kwa kazi, sio kwa maneno, sio kwa kugawa kanga kipindi cha uchaguzi na kuwarubuni Wajumbe, sio kwa kujipendekeza kwa Viongozi bali tukienda kwa Wananchi wakasema naam Mbunge wetu ndiye alipambania hii Shulea au Kituo cha Afya kikajengwa kauli hizo ndio zitafanya uteuliwe tena kupeperusha bendera ya CCM”


“Na kwenye ziara kote nitakakopita kama wewe Mbunge haufanyi kazi na hauonekani tunayo Timu ya kutosha kuchukua taarifa tutampelekea taarifa Mwenyekiti, kwamba Mwenyekiti tukienda na huyu tunapigwaa”



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/qeDykYS
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/g8FQoLO
Read More

Kiongozi ACT aliyepinga maandamano Chadema asimamishwa

January 20, 2024 0


Dar es Salaam. Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Dodoma, Yohana Mussa kwa madai ya kutoa kauli kinzani na msimamo wa chama hicho kuhusu miswaada mitatu ya sheria za uchaguzi.

Miswada hiyo ni ile inayohusu Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa iliyowasilishwa bungeni, Novemba 10 2023.

Mussa alikuwa miongoni mwa viongozi wa vyama kadhaa vya siasa  waaliozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kupinga maandamano ya Chadema yaliyopangwa kufanyika Januari 24.

Vyama hivyo ni ACT Wazalendo iliyowakilishwa na Mussa, CUF, NCCR Mageuzi, AAFP, ADC na Demokrasia Makini.

Siku moja ya tamko la vyama hivyo, ACT Wazalendo imetoa taarifa leo Januari 19, 2024 ikieleza kumsimamisha Mussa.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Naibu Katibu wa Habari Uhusiano na Umma wa chama hicho, Janeth Rithe, imesema  “Ndugu Yohana Mussa ambaye alitoa kauli kwa vyombo vya habari zinazokinzana na msimamo wa chama chetu kwenye miswada hiyo mitatu amesimamishwa uongozi na kutakiwa kujieleza.”

“Suala lake litapelekwa kwenye kikao kijacho cha Kamati Kuu kwa ajili ya maamuzi,” imeongeza taarifa hiyo bila kugusia suala la maandamano ya Chadema.


Taarifa hiyo imesema Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kitakutana Januari 27, 2024 kwenye kikao chake cha kawaida, ambapo pamoja na mambo mengine itafanya tathmini juu ya hali ya kisiasa nchini ikiwemo kuangazia mwenendo wa mambo ndani na nje ya Bunge kuhusu mjadala wa miswada hiyo.

Ameandika kuwa ACT Wazalendo ipo macho kufuatilia kwa karibu mwenendo wa mambo katika mjadala wa kitaifa unaoendelea kuhusu Miswada ya Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

“Chama chetu kilitoa rai kwa Serikali na Bunge kuhakikisha miswada hiyo inafanyiwa maboresho makubwa hasa kwa kujumuisha masuala ambayo tayari yalipata muafaka wa kitaifa na kukubalika na wadau wengi.

“Jopo la viongozi wa chama chetu likiongozwa na Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe liliwasilisha maoni yake mbele ya Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria. Ni imani yetu maoni hayo ambayo kwa hakika ndio maoni ya wadau wengi, yatazingatiwa.”

Mwananchi 


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/6jFse5d
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/umVLPvx
Read More

Friday, January 19, 2024

Matokeo ya Kidato cha Nne 2023-2024 Form 4 CSEE Results

January 19, 2024 0

 

Matokeo ya Kidato cha Nne 2023-2024 Form 4 CSEE Results


In this post find Matokeo ya Kidato cha Nne 2023-2024 Form Four CSEE Results, Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2023 Pdf, Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2023 Download, Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2023/2024, The most convenient and popular method is to check the results online through the NECTA website or other reliable portals.

As the academic year comes to an end, students in Tanzania are anxiously waiting for their NECTA CSEE results for the year 2023/2024. The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) is responsible for conducting exams for primary and secondary school students. If you are a form four student, you might have already taken the exams and waiting for your results. In this blog post, we will guide you on how to check your NECTA CSEE results 2023/2024. You can also download a PDF version of Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2023 NECTA Form Four Examination Results 2023/2024.

How to Check Your CSEE Results 2023/2024

Matokeo kidato cha nne 2023/2024

To check the Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024 online, you can visit the website of the National Examinations Council of Tanzania (NECTA). Simply navigate to the “CSEE Results” section and select the appropriate year click on the “Submit” button to view your NECTA CSEE examination results. By following these steps, you can easily access your NECTA CSEE results on-screen description. Also, you can check the CSEE necta results 2023/2024 using direct links provided below.

Matokeo kidato cha nne 2023/2024 and QT Results 2023/2024

 Frm four Results (NECTA CSEE results)

 QT Results

CSEE Results 2023-2024 Matokeo ya Kidato cha Nne 2023 A Step-by-Step Guide

There are several ways to check your NECTA CSEE Results for the year 2023/2024. Here are two methods you can use:

Method 1: Checking Results Online

  • Visit the official NECTA website at www.necta.go.tz.
  • Look for the “Result” or “Matokeo” section in the main menu and click on “CSEE Results.
  • Select the year of the exam as 2023.
  • Find your school in the provided list and locate your name.
  • Click on your name to view your results.
  • Save and print your results for future reference.

Method 2: Checking Results via SMS

  • Open the messaging app on your mobile phone.
  • Dial *152*00# to access the SMS service.
  • Select number 8 for “Elimu” (Education).
  • Choose number 2 for “NECTA.”
  • Select service type 1 for “Matokeo” (Results).
  • Enter your index number and examination year in the format “NECTA 123456 2023.”
  • Select the payment type (the cost per SMS is Tshs 100).
  • Wait for a reply from NECTA, which will include your exam results.

By following the steps outlined above, you can easily check your CSEE results (Matokeo kidato cha nne 2023/2024) from the National Examinations Council of Tanzania (NECTA) website. Be sure to keep a copy of the results for your records.

Can You Get NECTA Form Four Results 2023/2024 Via SMS/USSD Code?

Yes, it is possible to receive the NECTA Form Four Results 2023/2024 via SMS, and it is considered the best way to check your CSEE Results easily, faster and smoothly. By dialing the special USSD code provided by NECTA, *152*00#, and following the on-screen description, you can access your results. Please note that standard SMS charges may apply. This option offers a quick and convenient way to access your results.

ALSO READ:



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ze7Jmc9
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/xe7opcq
Read More

AFCON 2023: Misri Wapambana Kufa Kupona na Kulazimisha Sare ya 2-2 Dhidi ya Ghana

January 19, 2024 0
 

Misri ilipambana mara mbili na kupata sare ya 2-2 dhidi ya Ghana katika kipindi cha pili cha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika jijini Abidjan
Licha ya Ghana kuchukua uongozi kupitia kwa Mohammed Kudus na baadaye Omar Marmoush kuisawazishia Misri, Kudus wamerejesha uongozi wa Ghana haraka kwa juhudi zilizotoka nje
Bao la Mostafa Mohamed liliihakikishia Misri pointi yake ya pili, na kuiacha Ghana bila ushindi baada ya michezo miwili ya Kundi B, na timu zote mbili zikisubiri hatima yao katika mzunguko wa mwisho wa mechi
 

Misri ilirejea mara mbili na kupata sare ya 2-2 dhidi ya Ghana katika kipindi cha pili cha nguvu kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika jijini Abidjan. Awali Ghana walichukua nafasi ya kwanza huku Mohammed Kudus akifunga, lakini Omar Marmoush akaisawazishia Misri. Kwa haraka Kudus alirudisha uongozi wa Ghana, lakini bao la Mostafa Mohamed lilisawazisha tena bao hilo, na kuwaacha Ghana bila ushindi wowote baada ya michezo miwili ya Kundi B.

Kuumia kwa nahodha wa Misri, Mohamed Salah, ambaye alilazimika kutolewa nje katika kipindi cha kwanza, kunaleta wasiwasi kwa Waafrika Kaskazini na Liverpool. Kukosekana kwa Salah kulionekana katika mchezo huo, na kiwango cha jeraha bado hakijajulikana. Kocha wa Misri Rui Vitoria alielezea matumaini kuwa suala hilo sio muhimu lakini akasema kwamba ni mapema kutathminiwa.

Kipindi cha pili kilishuhudia bao la Mohamed Abdelmonem lililokataliwa kwa Misri kutokana na kuotea, na baadaye, Marmoush alitumia vyema mpira wa nyuma na kusawazisha. Hata hivyo, Ghana walipata tena bao la kuongoza kupitia kwa Kudus kabla ya Trezeguet kumtengenezea Mohamed bao la pili la kusawazisha Misri. Sare hiyo inaziacha Misri na Ghana zikiwa na majukumu mbele katika michezo yao ya mwisho ya makundi, huku Ghana ikiwa kwenye hatihati ya kufuzu kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Afcon.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/cIMD2jZ
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/d3INOs5
Read More

Binti atupa kichanga chooni hospitalini akihofia kuachika

January 19, 2024 0



Katavi. Rehema Erick (19) mkazi wa Kijiji cha Mtapenda Halmashauri ya Nsimbo ametupa mtoto chake kichanga cha siku moja chini ya sinki la kunawia mikono kwenye choo cha hospitali ya Nsimbo muda mfupi baada ya kujifungua, akihofia kuachwa na mume wake.

Akisimulia kisa hicho leo, Alhamisi Januari18, 2024 Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya halmashauri hiyo, Glory Solo amesema Rehema alifika hospitalini hapo akilalamika anasumbuliwa na maumivu ya tumbo.

Amesema daktari aliyemuona alimwandikia baadhi ya vipimo na baadaye Rehema alitoweka pasipo kufahamu alikoelekea jambo lililomfanya ndugu yake aliyempeleka hospitalini hapo naye kuanza kumtafuta.

"Kumbe aliingia chooni akawa amejifungua huyu mtoto na kisha alitoa kondo la nyuma na akamfunika mtoto kwenye kanga aliyokuwa nayo na kumsukumia nyuma ya sinki.

"Sisi tumegundua baada ya kumuona anatoka chooni akiwa anavuja damu nyingi, tulianza kumhudumia bila kujua baadaye watu walimleta mtoto wakadai ametupwa chooni, tulimuuliza akakana siyo wake," amesema Glory na kuongeza:

“Baadaye tulipoangalia mazingira yake ikiwemo kumhoji kwa kuwashirikisha Ustawi wa Jamii na vyombo vya sheria alikubali mtoto ni wake”.

Amesema madhara aliyopata mtoto kutokana na kuzaliwa katika mazingira hatarishi ni michubuko na amevunjika miguu yote miwili sehemu za mapaja.


Hata hivyo amesema mama na mtoto wote wanaendelea vizuri na matibabu huku mtoto akinyonya vizuri.

Rehema Erick anayedaiwa kuhusika na tukio hilo, alipoulizwa kwa nini amefanya kitendo hicho amesema amemtupa mtoto huyo kwa kuwa anahofia kuvunja ndoa yake kwakuwa aliolewa akiwa mjamzito.

"Nikuja kutibiwa juzi kabla ya kupimwa nilimuuliza muuguzi chooni ni wapi akanionyesha nikaenda nikakifungua nikamuacha mtoto kwa sababu niliolewa nikiwa na mimba na mme wangu angenifukuza," amesema Rehema.

Mume wa Rehema, Ramadhan Mrisho amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo ameshangaa uamuzi uliochukuliwa na mkewe kwani hakujua kama ni mjamzito.

"Ni miezi miwili tu tangu nimuoe akitokea Dar es Salaam, nikamchukua sijafunga naye ndoa alinificha maana mimba ilikuwa haionekani na baada ya kumuoa alisema yupo kipindi hatari anaweza kupata ujauzito.

"Nimejitambulisha kwao hatua ya kwanza, maandalizi ya kuchukua mahari yalikuwa yanaendelea, uamuzi wangu kwa sasa nitalea mtoto japo amenisikitisha sana kwa kumtupa," amesema Mrisho.

Ameongeza kuwa baada ya kufika hospitalini hapo hajamkaripia mkewe isipokuwa amemuuliza kama mtoto ananyonya na alijibiwa kuwa anasumbua.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yussuf amelaani  kitendo hicho  na akitoa onyo kwa wengine kuacha tabia hiyo ya ukatili.


"Serikali haitavumilia kamwe ukaliti wa aina hii, Jeshi la Polisi Mpanda nawaagiza kuchukua hatua kali za kisheria kwa binti huyu na wengine wanaoendekeza vitendo vya kikatili," amesema Jamila.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/oa6jHQA
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/nfQMue8
Read More

Thursday, January 18, 2024

Diamond Platnumz na Zuchu Ndio Basi Tena, Atangaza Yupo Single Kupitia Instagram

January 18, 2024 0



Star Wa Muziki Africa Diamond Platnumz Atangaza Rasmi Kuwa Kuanzia Leo Yupo Single Na Wala Hana Mahusiano Na Mwanamke Yeyote Yule Mpaka Pale Atakapowatambulisha Penzi Lake Jipya !. Diamond Amethibitisha Hilo Katika IG Story Yake Na Kisha Kuifuta Post Hiyo

from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/JIT9SBc
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/NiKBejY
Read More