Wakati kelele za tozo ya miamala ya simu zikiendelea kuanzia Agosti mwaka huu, watumiaji wa simu nchini wataanza kuchangia bajeti kuu ya Serikali kupitia tozo ya laini za simu kwa kila anayeongeza salio la maongezi.
Tayari watoa huduma wamekuwa wakilalamikia kodi kubwa katika vocha za simu ambapo inaelezwa kuwa kodi za Serikali hufikia hadi asilimia 40 ya salio analoweka mteja.
Katika bajeti iliyopitishwa na Bunge Serikali ilipanga kutoza kiasi cha Sh10 hadi Sh200 kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji. Serikali ilisema kupitia tozo hiyo itakusanya kiasi cha Sh396.3 bilioni kwa mwaka huu.
Kutokana na pendekezo la tozo hiyo ambayo Serikali imekuwa akisisitiza kuwa kodi ya mshikamano kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, hivi karibuni Serikali imetoa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa makato hayo ambayo huenda nayo yakaleta kilele miongoni mwa watumiaji.
Kanuni zilizopelekwa kwa watoa huduma za simu kwa ajili ya kuanza utekelezaji ifikapo Agosti mosi zinaonyesha kuwa kila laini ya simu itatozwa Sh5 pindi itakapoongezewa salio lisilozidi Sh1,000 na itatozwa Sh223 kwa kuongeza salio linalozidi Sh100,000.
Kwa anayeongeza salio la Sh1,001 hadi Sh2,500 atatozwa Sh10, Salio la Sh2,501 hadi Sh5,000 tozo mpya ni Sh21, Salio la Sh5,001 hadi Sh7,500 tozo mpya ni Sh40, salio la Sh7,501 hadi Sh10,000 tozo mpya Sh76, Salio la Sh10,001 hadi Sh25,000 tozo mpya Sh113, salio la Sh25,001 hadi Sh50,000 tozo mpya Sh153 na salio la Sh50,001 hadi Sh100,000 tozo itakuwa Sh186.
Ofisa mmoja mwandamizi wa kampuni ya huduma za simu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazeti aliliambia gazeti hili kuwa mpaka sasa majadiliano yanaendelea juu ya namna ya kutoza kodi hizo, lakini kuna uwezekano mkubwa zikabebwa nje ya vifurushi.
“Mpaka sasa mwelekeo ni kuzibeba tozo hizo nje ya vifurushi kwa kuwa sisi ni wakusanyaji tu huwezi kuzimeza, tukizimeza thamani ya vocha husika itapungua, yaani kwa mfano Sh500 itakuwa na thamani ya Sh495, hivyo tukizimeza itabidi kifurushi kilichokuwa cha Sh500 kitolewe kwa Sh495 au tukibadilishe kiwe na thamani ya Sh495 na hilo sio sawa,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alisema athari za kumeza kodi hiyo ni kupunguza wastani wa matumizi ya mteja kwa siku, hivyo kama kwa Sh500 mtu alikuwa anapata dakika 8, tutamlazimisha sasa kutumia pungufu kulingana na thamani ya fedha yake itakayokuwa imebaki, ndiyo maana mpaka sasa njia iliyopo ni kuibeba tozo hiyo nje ya vifurushi vyetu.
“Kwa utaratibu huo sasa ili kupata kifurushi cha Sh500 lazima uongeze Sh505, vivyo hivyo kwa vifurushi vingine ili upate kifurushi fulani ni lazima uongeze salio linalofikia thamani ya kifurushi hicho pamoja na tozo, tofauti na hapo salio lililowekwa halitatosha kujiunga kwa kuwa litakatwa tozo. Itakuwa hivyo hata mtu atakayetaka kujiunga kupitia akaunti za miamala ya simu kama huna zaidi kifurushi hakitakubali,” alisema.
Dickson Joseph ambaye ni mtumiaji wa simu alisema kutokana na utitiri wa tozo katika siku hivi sasa kifaa hicho cha mawasiliano hakitatumika sana kama ilivyo sasa na badala yake kitatumika tu pale penye ulazima sana.
from Udaku Special https://ift.tt/3ipKU59
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3wNIna3
No comments:
Post a Comment