Kesi ya muda mrefu ya rushwa inayomkabili rais wa zamani wa Afrika Kusini aliyeko jela Jacob Zuma itaendelea leo kwa njia ya video, licha ya vurugu kali ambazo zimelikumba taifa hilo baada ya kufungwa jela katika kesi nyingine.
Zuma anakabiliwa na mashitaka 16 ya ulaghai na rushwa kuhusiana na ununuzi wa mwaka wa 1999 wa ndege za kivita, boti za kushika doria na vifaa vya jeshi kutoka kwa kampuni tano za kijeshi barani Ulaya wakati akiwa naibu wa rais. Anatuhumiwa kupokea hongo kutoka kwa moja ya kampuni hizo, Thales ya Ufaransa, ambayo ilishitakiwa kwa rushwa na utakatishaji pesa.
Kesi hiyo ilianza Mei baada ya kuahirishwa na kucheleweshwa mara nyingi, wakati timu ya utetezi ya Zuma ikipambana kutaka mashitaka hayo yafutwe. Zuma mwenye umri wa miaka 79, anasisitiza hana hatia. Kampuni ya Thales pia ilikana mashitaka.
from Udaku Special https://ift.tt/3zfPnho
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3ioHv6B
No comments:
Post a Comment