Wallace Karia Apitishwa na Kuwa Mgombea Pekee wa Urais TFF - Mapenz Wakubwa

Hot

Tuesday, June 29, 2021

Wallace Karia Apitishwa na Kuwa Mgombea Pekee wa Urais TFF





Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo Juni 29, 2029 imempitisha Wallace Karia kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Rais wa shirikisho hilo, baada ya kukidhi vigezo vyote.
Wallace Karia ambae ndio Rais wa sasa wa TFF jina lake pekee ndio lililopitishwa na kamati ya uchaguzi, baada ya wagombea wengine wa nafasi hiyo ya Urais Hawa Mniga pamoja na Evance Mgeusa kukosa vigezo vinavyokidhi kwa wao kuendelea na hatua inayofata kwenye uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Benjamini Kalume amesema kwa sasa kitakachofanyika ni Wallace Karia akiwa kama mgombea pekee ni kwenda kuthibitishwa na Mkutano mkuu na si kumpigia Kura.

Mkutano Mkuu wa TFF utafanyika Agosti 7, 2021 Mkoani Tanga ambapo moja ya Ajenda ya mkutano huo ni Uchaguzi wa kuchagua viongozi wa shirikisho hilo ikiwemo nafasi ya Urais na nafasi sita (6) za wajumbe wa kamati ya Utendaji.
 



from Udaku Special https://ift.tt/3jlUaJH
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/3qzdIM3

No comments:

Post a Comment