Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslimu amesema mmiliki wa gari lililosababisha vifo vya watu tisa iliyotokea eneo la Oil com, Nanenane Manispaa ya Morogoro amejisalimisha polisi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, Juni 29, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye kituo kikuu cha Mabasi Msamvu wakati wa Operesheni maalumu ya ukaguzi wa Mabasi ya abiria.
Kamanda Muslimu amesema katika operesheni hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo,wamekamata magari 36 ambayo hayakuwa na vibali vya kusafiri.
Aidha,amebainisha kuwa magari mengi yamekuwa yakiwekwa mashada ya maua na picha zinazoonyesha kuwa ni za marehemu huku wahusika wakieleza kuwa wanasafirisha msiba wakati wanajua kuwa si kweli
from Udaku Special https://ift.tt/2Ucl8sN
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3hgILZ0
No comments:
Post a Comment