Paula Aanza Vijembe "Kwangu Habanduki Kwako Hatoboki…Jamani Wambeya Habari zenu Muwe na Siku Njema“ - Mapenz Wakubwa

Hot

Sunday, March 6, 2022

Paula Aanza Vijembe "Kwangu Habanduki Kwako Hatoboki…Jamani Wambeya Habari zenu Muwe na Siku Njema“


PAULA Kajala @therealpaulahkajala ; ni binti wa mwigizaji wa Bongo Movies, Kajala Masanja au Frida na prodyuza wa Bongo Records, P Funk Majani ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Uturuki akisomea masomo ya uuguzi.


Paula amekuwa maarufu zaidi baada ya kujulikana anatoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Rayvanny @rayvanny akimpokonya Fayhma tonge mdomoni.


Amekuwa akiwarushia vijembe watu wanaomsakama kwamba alimchukulia Fayhma mtu wake ambapo safari hii amerusha kijembe kingine akimaanisha kwamba mwanaume wake hawezi kubanduka kwake.

Kupitia Insta Story yake, Paula ameandika; “Kwangu habanduki kwako hatoboki…jamani wambeya habari zenu muwe na siku njema. “


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/XZCMTIo
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/MSFb5Wn

No comments:

Post a Comment