Rapa Wakazi ameanika wazi baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakikwamisha muziki wetu. Kwenye mahojiano na kipindi cha EMPIRE @efmtanzania jana Jumatano, Wakazi alisema mbali na athari za COVID-19, ujio wa wadau wa muziki kama makampuni makubwa na Record Labels, tatizo kubwa ambalo limeathiri muziki wetu ni ushindani usio na tija baina ya wasanii.
"Kitu ambacho kimeumiza game yetu ambacho hakikupaswa ni ushindani usio na tija. Hii inasababisha mashabiki wanagawanyika, watu wanaacha vitu vya msingi kama kukuza brand, wanaanza kupondeana wenyewe kwa wenyewe."
"Hiyo kidogo inaturudisha nyuma na hatushindanii muziki, tunashindania Mimi ni kitu gani, Mimi ninatoka na nani. Tunapoteza focus ya ushindani ya kutoa kazi bora, tunaanza kuonesha mara sijui mimi nina Trend, sio wimbo mzuri ila ilimradi tu ina-trend. Hiyo inatuumiza kiusanii na tunashindwa kushindana Kimataifa." alimaliza @wakazi
from Udaku Special https://ift.tt/3wPWiN2
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3kp9ju5
No comments:
Post a Comment