WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema hadi sasa jumla ya watu 29 wamefariki dunia kutokana na wimbi la tatu la Covid-19 huku jana Julai 22, 2021 pekee kulikuwa na jumla ya wagonjwa wapya 176.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 23, 2021, Dkt. Dorothy amesema takwimu hizo ni alizopata jana hivyo upo uwezekano vifo zaidi vikawa vimetokea.
“Itoshe kuwaambia kuwa ugonjwa upo na watu wanakufa, tusingependa kupeana hizi taarifa za vifo tuchukue tahadhari, kila mmoja wetu ajiulize unapofanya mambo kinyume na kuchukua tahadhari unalenga kumtesa nani,” amesema Dkt. Gwajima.
Idadi hiyo inafikisha Tanzania kuwa na jumla ya wagonjwa 858 wa Covid-19. Waziri ameeleza kuwa licha ya Serikali kuendelea kusisitiza watu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo bado wapo wanaozembea. Waziri huyo pia alitupa lawama kwa viongozi wa Serikali ambao hawashiriki kwenye vita vya kupambana na ugonjwa huo.
“Nawakumbusha watu hawa wasiotaka kwenda mstari wa mbele wasichukulie mzaha Uviko 19, ugonjwa huu upo tusijiachie kwa sababu wimbi la kwanza na la pili lilipita,” amesema Gwajima.
from Udaku Special https://ift.tt/3l2dcFZ
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3ByOkvi
No comments:
Post a Comment