Mhandisi Patrick Aron Lipilima Mfugale, Alizaliwa katika eneo la Ifunda, mkoa wa Iringa na Alisoma elimu ya Msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School iliyopo Iringa mjini . 1975 Alimaliza elimu yake ya Sekondari huko Moshi.
Alipata Shahada ya kwanza ya Uhandisi mwaka 1983 kutoka Chuo Kikuu cha Rokii (Nchini India) iliyofuatwa na shahada ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Loughbrough (Nchini Uingereza) mwaka 1995.
Aliajiriwa Wizara ya Ujenzi kama fundi sanifu mwaka 1977, na kutokana na utumishi wake uliotukuka,Juhudi na nidhamu alipanda kutoka fundi sanifu mpaka Mkurugenzi wa bara bara za Mikoa mwaka 1992.
Aliteuliwa kuwa Muhandisi mkuu wa Madaraja nchini Tanzania wakati huo, na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja hapa nchini.
Alitengeneza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina la “Tanzania Bridge Management System”
Alisajiliwa kama Mhandisi mtaalamu (yaani Proffessional Engineer) mwaka 1991 na namba yake ya usajili ilikua ni 689.
Amekua mjumbe wa bodi mbali mbali katika utumishi wake zikiwemo NCC, Road Fund Board ,MEKO na nyingine nyiingi.
Injinia Mfugale ametumia muda wake mwingi sana wa utumishi kama mtaalamu wa madaraja nchini.
Mfugale huyu huyu ndie Aliebuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa muda wa miezi 3 kwa shilingi za Tanzania milioni 300 wakati huo,Na kupunguza umbali wa kutoka Tabora hadi kugoma,kutoka kilomita 760 hadi kilomita 420.
Injinia mfugale ameshiriki akiwa kiongozi wa wataalamu katika kusanifu na kujenga madaraja makubwa mbali mbali kwa uchache Daraja la Mkapa kwenye mto Rufiji,Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji, daraja la Rusumo mkoani Mara, daraja la Kikwete, kwenye mto Malagarasi, daraja la Nyerere Kigamboni,Daraja la Kijazi lililopo ubungo Mkoani Dar es Salaam na madaraja mengine makubwa yaliyopo katika hatua mbali mbali.
Injinia Patrick mfugale Akiwa mhandisi mkuu katika iliyokua Wizara ya Ujenzi ameongoza katika kubuni na kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa na madogo yapatayo 1400 hapa nchini.
Imeandikwa kwa Ushirikiano wa; Bakari Waziri na Yasini Ng’itu
from Udaku Special https://ift.tt/3qIuHvr
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3qERLLR
No comments:
Post a Comment