Mavoko Afichua Siri "Diamond Platnumz Hakuwa Rafiki" - Mapenz Wakubwa

Hot

Tuesday, July 20, 2021

Mavoko Afichua Siri "Diamond Platnumz Hakuwa Rafiki"



Msanii wa Bongof Fleva, Rich Mavoko amedai kuwa hakuwahi kuwa na ushikaji wala urafiki na Diamond Platnumz licha ya kusainiwa kwenye lebo yake, WCB Wasafi.

Akihojiwa na Willy M Tuza kwenye kipindi cha Mambo Mseto kinachoruka Radio Citizen, Kenya, Mavoko amesema hata kujiunga kwake kwenye lebo hiyo ni Diamond alimtumia watu.

"Hatukuwa kuwa washikaji, na hata tulipokuwa kwenye lebo hatukuwahi kuwa marafiki," amesema Mavoko ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake mpya, Nidonoe.

"Sikuwahi kumtafuta mtu kufanya naye kazi kwa sababu nilikuwa na kipaji sana. Nilitafutwa na watu wengine ambao yeye aliwatuma, alishindwa kuni-face, I think," amesema Rich Mavoko.

Pia Mavoko amesema licha ya kutamba na kuwa msanii mkubwa kabla ya kusaini WCB Wasafi, si sawa kushindanishwa na Diamond kwani wakati anatoa albamu yake ya kwanza, Kwamwambie (2010) yeye alikuwa Kidato cha Nne, hivyo wamepishana kiumri ndani ya muziki.


from Udaku Special https://ift.tt/2UkUa2F
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/3xR6s0Y

No comments:

Post a Comment