Kumekucha..Simbachawene Amtaka Bosi wa NIDA Ajitathimini - Mapenz Wakubwa

Hot

Tuesday, July 20, 2021

Kumekucha..Simbachawene Amtaka Bosi wa NIDA Ajitathimini




Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, amesema tangu ameanza kupiga kelele kuhusu vitambulisho vya NIDA hadi sasa vilivyozalishwa ni milioni 2 tu na kusema hali hiyo hawezi kuivumilia, na kumuambia Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Anold Kihaule, kama kazi imemshinda aseme.
Kauli hiyo ameitoa akiwa mkoani Iringa, na kumtaka Mkurugenzi huyo ajitathimini kuhusu suala la vitambulisho na kwamba kama anaona hawezi basi amwambie Rais Samia Suluhu Hassan, kama ameshindwa kazi hiyo ili nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine.

"Kwahiyo tangu nimeingia kwenye uwaziri kelele zote nilizopiga kwenye vitambulisho zimezalisha vitambulisho milioni 2 tu, na mimi siwezi kukubali ninachomwambia huyo Mkurugenzi Mkuu kama hii kazi imemshinda apewe kazi nyingine na hii aachie watu wengine, sawa ni mteule wa Rais, kama imemshinda amwambie," amesema Waziri Simbachawene.


from Udaku Special https://ift.tt/3eBqeWQ
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/2W2r5ta

No comments:

Post a Comment