Ghasia za Afrika Kusini: Ni nini chanzo cha ghasia na uporaji? - Mapenz Wakubwa

Hot

Saturday, July 17, 2021

Ghasia za Afrika Kusini: Ni nini chanzo cha ghasia na uporaji?




Baadhi wanayaita matukio yaliyotokea wiki iliyopita kama ''kipindi cha giza'' cha Afrika kusini yenye demokrasia.


Lakini je ni zaidi ya kuzuka ghafla kwa hasira kulikosababishwa na kufungwa kwa rais wa zamani Jacob Zuma? Wachambuzi wengi wanasema ni kweli kwamba kuna "msukumo wa tatu " wa huruma kwa rais huyo wa zamani unaohusika.



Lugha ya serikali pia imebadilika kwa kiasi kikubwa, kutoka kutosema mengi katika siku za mwanzo za ghasia hadi kutoa wito wa kile inachosema kimekuwa ni "uhujumu uchumi ".



Baadhi ya wadadisi wameonya kuwa ghasia zimekuwa na dalili ya "jaribio la mapinduzi" na "mwamko wa mageuzi dhidi ya serikali".



Rais Cyril Ramaphosa amesema kuwa ghasia zilipangwa lakini hajasema ni nani alichochea a ghasia hizo .



Mhariri msaidizi Ferial Haffajee, wa gazeti la Daily Maverick, ameandika kuhusu mkakati ulio[pangwa wa ghasia, uliopangwa na washirika kumi na wawili wa rais huyo



Akimaanisha vyanzo vya maafisa kadhaa ndani ya ndani ya chama tawala cha African National Congress (ANC) na huduma za ujasusi , Haffajee ameainisha muundo wa mkakati huo- kuanzia kuteketea wa malori ya uchukuzi KwaZulu-Natal ulioshuhudiwa siku za mwanzoni mwa ghasia, hadi kufungwa kwa barabara muhimu inayotoka Durban hadi katika kitovu cha uchumi wa Afrika Kusini , Gauteng.



Maelezo ni kwamba hii ililenga kwa makusudi kudhoofisha zaidi uchumi ambao tayari ni dhaifu.



Hii inaweza kuwa inatoka ndani ya chama tawala na huduma za taifa za ujasusi kwa pamoja.



Kuna nguvu mbili zinazopingana wazi ndani ya chama cha ANC. Moja inaongozwa na Rais Ramaphosa, ambaye wafuasi wake wanasema taratibu anajenga upya taasisi za taifa baada ya muongo wa ufisadi na uporaji wakati wa utawala wa Zuma. Na mwingine kutoka kwa kikundi kinachofahamika kama RET , kinachomuonea rais wa zamani Jacob Zuma na wafuasi sugu wa rais wa zamani Jacob Zuma.



Huenda walinufaishwa na "kukamatwa kwa taifa " kwa Bw Zuma na wanahisi wametengwa na kasi ya kikundi cha Ramaphosa. Wanataka mabadiliko ya uongozi haraka na wana nufaika iwapo rais wa sasa amedhoofishwa.



Zuma alikuwa mkuu wa ujasusi maarufu sana wa ANC ndani na nje ya Afrika Kusini wakati wa enzi ya utawala wa Wazungu , kabla ya kupata ushindi mwaka 1990. Karibu miaka minne tangu aondoke madarakani, anaaminiwa kudumisha ushirika imara katika huduma za ujasusi nchini humo.



Hilo halishangazi. Wakati wa muhula wake madarakani kiasi kikubwa cha fedha kilielekezwa katika mwelekeo huo. Ukweli ni kwamba, kile kilichojitokeza katika tume ya uchunguzi wa ufisadi uliofanyika wakati wa urais wa Bw Zuma kinaonesha kwamba wakati wa miaka yake mamlakani, mifumo ya ujasusi iliundwa kando ya ile iliyokuwepo ikitekeleza matakwa ya rais.



Kama hilo ni kweli, mabaki ya miundo hiyo kweli bado yapo. Profesa Susan Booysen anasema kwamba licha ya ripoti ya mwaka 2018 kutambua "mifumo ya kando ya ujasusi" yenye uwezekano wa kuegemea au yenye huruma kwa rais wa zamani, ni machache yaliyofanywa na utawala wa sasa katika kuyang'oa makundi haya . Tunaweza kuwa tunashuhudia athari zake sasa.



Washirika na wafuasi wa Zuma wanakana hili, wakisema kuhusisha makundi hayo na siasa katika mapambano au mifumo ya ujasusi ni jaribio la kuficha kushindwa vibaya kwa serikali katika utoaji wa huduma kwa masikini , pamoja na kubashiri na kushugulikia matukio ya ghasia.



Hakika jibu la serikali lilicheleweshwa na la ghafla - na lilikuwa kubwa kutokana na hilo.



Tangazo la ombi kwa ajili ya vikosi 25,000 vya ziada kwa miezi mitatu linapaswa kueleweka katika muktadha wa historia ya Afrika Afrika Kusini. Halikuwa la kawaida na ni kikosi kikubwa kuwahi kupelekwa kwenye maeneo ya Afrika Kusini tangu mwishoni mwa utawala wa ubaguzi wa rangi.



Huku bado katika siku za kuelekea kutolewa kwa tangazo hili, uongozi wa kisiasa na kijeshi nchini humo ulisikika ukisitasita wazi kupeleka wanajeshi zaidi - kando na kutangaza "hali ya dharura ya taifa ".



Hili halishangazi, kuona kile kinachotokea nchini humo.



Katika mkutano maafisa wa juu wa usalama, waliwakumbusha raia wa Afrika Kusini kwamba wanajeshi hawako pale kutekeleza sheria, hiyo ni kazi ya polisi.



Hii ilikubalika katika utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini uliotangaza hali ya tahadhari katika miaka ya katikakati mwa -1980 wakati nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa sheria ya kijeshi.



Matumizi ya jeshi ni jambo linaloweza kuleta hisia za juu . Kwamba wamewapeleka wanajeshi kadhaa kwamba wameonyesha ukubwa wa hali.



Hii imeonesha wazi kwamba ni zaidi ya kudhibiti uporaji , na kwamba kuna haja ya kulinda maisha na maslahi ya taifa kama vile bandari ya Durban, hifadhi ya mafuta, mitandao ya mawasiliani na biashara muhimu pamoja na mifumo ya usambazaji wa chakula na mafuta - vyote ambavyo vimetishiwa au kushambuliwa.



Kuna watu binafsi kadhaa ndani ya ANC na katika huduma za ujasusi za nchi wanaopoteza mengi iwapo kutakuwa na uwajibishwaji na utawala wa kisheria, kama ilivyotokea mapema mwezi huu wakati rais wa zamani alipofungwa na Mahakama ya katiba.



Kutokana na msukumo unaotokana na ukosefu wa usalama, kumekuwa na upungufu wa chakula na mafuta. Inaonekana dhahiri kwamba athari za ukosefu wa ajira ndizo zinazosababisha haya.



from Udaku Special https://ift.tt/3xQS1dw
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/3hMafqY

No comments:

Post a Comment