Asilimia 60 ya Watanzania Kuchanjwa, Watakaoanza ni Hawa - Mapenz Wakubwa

Hot

Wednesday, July 28, 2021

Asilimia 60 ya Watanzania Kuchanjwa, Watakaoanza ni Hawa



Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Gerson Msigwa amesema kuwa chanjo za homa ya virusi vya corona inayosababisha homa ya mapafu zilizoletwa nchini zinakidhi asilimia 20 ya idadi ya wananchi wote wa Tanzania huku mpango wa Serikali ni kutoa chanjo kwa watu takriban asilimia 60.

Msigwa amesema hayo leo wakati akizungumza na moja ya chombo cha habari nchini na kupitia ukurasa wake wa Twitter; “Chanjo zilizoletwa zinakidhi asilimia 20 ya idadi ya wananchi wote, mpango wa Serikali ni kutoa chanjo kwa watu takriban asilimia 60 kwa hiyo Serikali itaendelea kufanya utaratibu wa kuhakikisha asilimia 40 zilizobaki zinapatikana.

“Wizara ya Afya imeandaa utaratibu ambapo kati kipindi cha kati ya siku ya 7 – 10 itakuwa kwa ajili ya makundi yaliyopewa kipaumbele yakiwemo ya wafanyakazi wa afya wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi na watu wenye umri mkubwa.

“Kusaini Hati ya Tiba ni jambo la kawaida nchini, kwa Chanjo ya UVIKO-19 haitakua jambo geni, hata ukienda kufanyiwa upasuaji wowote huwa unasaini, tuache upotoshaji. Niwatoe hofu Watanzania kuwa wataalam wetu wanaendelea kuzihakiki chanjo hizi, hili tatizo la UVIKO-19 ni la dunia nzima, natoa wito kwa Watanzania kuwasikiliza wataalam kama nchi nyingine zinavyofanya.


 
“Shughuli za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya zinaendelea kama kawaida, Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Kenya imekua na matokeo chanya kero nyingi, hususan za kibiashara zimetatuliwa.

“Ugonjwa wa UVIKO-19 upo, tuendelee kuchukua tahadhari na kufuata muongozo wa UVIKO-19 uliyotolewa na Mamlaka. Aidha, natoa rai kwa Watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Samia kwa kuendelee kuchapa kazi.

“Suala la tozo za miamala ya simu limeanza kufanyiwa kazi, taratibu zinakamilishwa na mwisho wa mwezi Julai Serikali itakuja na majibu,” amesema Msigwa.


from Udaku Special https://ift.tt/3iYVUGK
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/3ycT1IV

No comments:

Post a Comment