Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Muslimu amesema mmiliki wa gari lililosababisha vifo vya watu tisa eneo la Nanenane manispaa ya Morogoro amejisalimisha polisi.
Kamanda Muslimu ameyasema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Msamvu, ilipofanyika operesheni maalumu ya ukaguzi wa mabasi ya abiria ambapo amesema katika operesheni hiyo iliyofanyika usiku, wamekamata magari 36 ambayo hayakuwa na vibali vya kusafiri.
from Udaku Special https://ift.tt/3y3usxv
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3juCLyr
No comments:
Post a Comment