Mange ni Noma..Amkalisha Kiti Moto Mama Dangote Kuhusu Tabia za Diamond Platnumz "Ninyi Mnaomzunguka Mwambieni Abadilike" - Mapenz Wakubwa

Hot

Tuesday, June 29, 2021

Mange ni Noma..Amkalisha Kiti Moto Mama Dangote Kuhusu Tabia za Diamond Platnumz "Ninyi Mnaomzunguka Mwambieni Abadilike"

 


Kaandika Mange Kimambi:

Sijawahi kucomment humu ila leo imebidi. Mama umezaa the best artist in East and Central Africa. Anaekataa hilo ni taahira. Ila mama inabidi nyinyi mnaomzunguka mumsaidie abadilike na nyinyi pia mbadilike. Haiwezekani achukiwe kiasi hiki, kuna tatizo kwenye upande wenu. Mungu kamsaidia kafanikiwa sasa kwanini mtumie baraka hizo kurusha watu roho na kumjengea kijana chuki kila kona? Mama naomba upite blog zote za wanaigeria ni wamemposti mtu wao kwa nidhamu. Hakuna majigambo. Hakuna chawa wa Burna Boy anaetukana watu. Burna Boy mwenyewe hata kuposti hajaposti mpaka sasa na nnaamini hata akiposti ataandika mistari mitatu ya hekima basi. Ila angeshinda mwanao mngeringa, mmengesenya watu, mngejishaua mpaka watu wakasirike. Mimi nilikuwa nataka ashinde ila pia nilishajifunga kibwebwe nikisubiri vichambo. Kwanini iwe hivyo? Tafadhali badilieni. Mwanao ndo tegemeo letu kwa sasa hivi la kuwashinda wanaigeria kwa hiyo acheni kumjengea chuki na watu ambae wangekuwa fans wake na kumuongezea utajiri. Hao machawa hawamsadiiii kitu zaidi ya kumjengea chuki. Alafu mwanao hakuwaga hivi zamani, Ila toka wasafi tv and radio vianze ndo kabadilika mnoooooo. Na huwezi kusema machawa ndo walaumiwe sababu kumbuka mwanao huwa anasimama hadharani anawapa na zawadi kwahiyo ni anakubaliana na kila wanachofanya. Tafadhali badilikeni.

Naomba nikupe mfano mdogo. Ile ya issue ya Forbes. Angeweza kuihandle vizuriii mnooo na kufunga midomo waliokuwa wanamcheka. Angesema tu siamini mimi mtoto wa maskini nilieuza mitumba leo jina langu lipo Forbes. Ahsante Mama kwa kunifikisha Forbes na Mimi leo nipo kwenye orodha ya mamilionea. Kweli mimi mtoto wa Tandale nna thamani ya mamilioni ya dola? Naseeb angesema hivyo ungeona jinsi kila kitu angebadilisha maneno na kuanza kumpongeza. Ila yeye akaja na kiburi. Alafu mameneja wake ni wajinga mnooo hawamsaidiiiii,meneja mwenyewe anapenda kuchambana ndo maana na Diamond amekuwa na tabia kama za meneja.

Please badilikeni.



from Udaku Special https://ift.tt/3x8b2HK
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/3h3YYln

No comments:

Post a Comment