Kauli ya Samia kuhusu bandari ya Bagamoyo - Mapenz Wakubwa

Hot

Sunday, June 27, 2021

Kauli ya Samia kuhusu bandari ya Bagamoyo

 


Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wa bandari ya Bagamoyo pamoja na kufufua mradi wa makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma kwa kuwa soko la chuma kwa Dunia limepanda.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 26, 2021, mkoani Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara.

"Kuhusu bandari ya Bagamoyo tumeanza mazungumzo ya kufufua mradi wote ule wa Bagamoyo pamoja na Mchuchuma na Liganga nilishatoa maelekezo nadhani sekta husika zinaendelea na mazungumzo kuona tatizo ni nini" amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa "Kuhusu Mchuchuma na Liganga mazungumza yanaendelea kuona tatizo ni nini serikali inaweza kujitoa mpaka wapi, mwekezaji ajitoe mpaka wapi na taarifa zilizopo Duniani chuma imepanda bei ni wakati mzuri wa kuharakisha na kufanya ule mradi"



from Udaku Special https://ift.tt/3A50v2b
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/35Uffmv

No comments:

Post a Comment