Haji Manara Awatakia Mafanikio Yanga Kuelekea Kwenye Mabadiriko - Mapenz Wakubwa

Hot

Tuesday, June 29, 2021

Haji Manara Awatakia Mafanikio Yanga Kuelekea Kwenye Mabadiriko

Msemaji wa timu ya Simba Haji Manara amewapongeza timu ya Yanga  nakuwatakia mafanikio mema kuelekea kwenye mabadiriko.

Anaandika Haji Manara Ofisa Habari wa Simba namna hii:- Sitegemei kusikia mizengwe ya wale waliokuwa wakikesha katika redio kupinga mabadiliko ya uendeshaji wa vilabu.

Yoyote mwenye kutaka mafanikio ya vilabu vyetu lazma aunge mkono mabadiliko ambayo Simba na Yanga wanavyotaka kuyafanya.

Wale waliokuwa wakiwatumia wapinga mabadiliko ya Simba na kuwaita kila siku kuwahoji tunawaomba wasifanye hivyo kwa wenzetu.

Na hatutegemei kuona simu zao kila siku kwenda FCC kuhoji mizengwe isiyo na faida yoyote kwa vilabu vyetu. Waache Wanachama walioamua kubadilisha mifumo wakamilishe dhamira zao njema.

Isije tena watu wale wale kuanza kutumika kuvuruga hivi vilabu kwa maslahi yao, maana huko wenzetu mna vigogo viwili, ikitokea mmoja akaslide kidogo tu,basi mtawaona wapika sumu!.

Hao hawakawii kuvuruga mambo, walau Simba ilishawachukulia kama machale tu, sasa nyie Yanga kaeni nao macho hao watu, hawana dini katika Bakhshishi na wapo tayari kufanya lolote lile ili mradi yao yatimie.

Ahhh tuachane na hayo, mimi nawatakia kila la kheri Watani zangu katika mabadiliko mliyoyaanza jana, najua huo ni mwanzo kwa vilabu vyote nchini kwenda na mifumo ya kisasa ya uendeshaji wa vilabu vya soka wenye tija kwetu.



from Udaku Special https://ift.tt/3x53HJb
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/3y2T5dH

No comments:

Post a Comment