"dada zangu samahani jamani kwani kuna nini mbona siwaelewi?" aliuliza Brown huku akiwa ameanza kukasirka "usikasirike kaka yangu sisi umetushngaza sana..." "nimewashangaza na nini? hivi dada ungekuwa wewe unaongea alafu watu wanakushangaa hivi ungejisikiaje?" "ni kweli kaka yangu naomba utusamehe kwa hilo lakini ngoja tumwite baba alafu umuulize Salma yupo wapi? alafu utaona atakavyo shangaa?" "hapana msimsumbue mzee nyie niambieni tu yupo ama hayupo?" "sawa ni hivi kaka yangu....samahani lakini Salma...mh ! yaani Salma alifariki miaka miwili iliyopita...." "nini? haiwezekani mh ! mh! kama kuna waongo duniani basi wewe umeshinda...atii?"
"huamini nenda kaulize hata hapo nyumba ya jirani" alisema mmoja wa wale madada "mh ! haina haja....siwezi kuamini mtu nilikuwa naye jana nimekuja naye mpaka chumbani kwake tena kanipa na mkufu huu wa dhahabu kama ishara ya mapenzi yetu alafu unasema..." Brown aliongea kwa hasira sana huku akitoa mfukoni ule mkufu "ni hivi Salma ni ndugu yetu kabisa...na ni kweli alifariki na chumba chake kipo humu ndani pamoja na vitu vyake na huo mkufu ni wake mimi naujuwa....." "sasa unasemaje amefariki tena miaka miwili ilyopita siwezi kukubali kirahisi",dada mkubwa wa wale madada alishauri labda Brown aonyeshe chumba alichokuja jana usiku.
Walinyanyuka na kuingia ndani,Brown alikwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Salma "hiki hapa chumba chake,ndani kuna kabati kubwa la nguo lenye vioo viwili,kitanda cha futi sita kwa sita,mabegi matatu ya nguo upande wa kushoto wa chumba yamebebana...." "mh ! kaka yangu unatuchanganya ujue...hebu ngoja tufungue" "sawa fungueni" mlango wa chumba ulifunguliwa,Brown,wale madada na baadhi ya majirani wakina msipitwe walikuja kushuhudia.dada mkubwa alienda mpaka kwenye kabati alifungua,hakuona mkufu "mh ! jamani mkufu haupo...hii sasa kali" "mimi nawaambia nilikuwa naye jana usiku club Billcanas nilimrudisha hapa nikaingia naye humu chumbani akanipa huu mkufu sasa mnaniona mwendawazimu kwa lipi?"
"hapana kaka yangu hatujakuona mwendawazimu ila mambo yanashangaza yaani mdogo wangu alifariki na mtaa mzima wanajua" aliongea dada mkubwa,mama moja alipendekeza "basi twendeni tukamuonyeshe kaburi labda ataelewa" "sawa twendeni" walitoka mpaka makaburi ya ilala mchikichini,walipofika walikuta juu ya kaburi koti la Brown na gauni jekundu alilovaa Salma jana usiku "mh ! hiki nini sasa au naota" alisema moyoni huku moyo ukimdunda kwa nguvu "haya sasa kaka sema kaburi la Salma hili hapa" aliongea dada mkubwa "sina la kusema dada yangu...hili koti ni langu nilimfunika nalo Salma jana usiku aliposikia baridi" "mh ! unasema kweli?" "sasa kwa nini niongope dada yangu tena nimekumbuka ndani ya mfuko wa koti kuna kadi yangu ya benki" walipoangalia waliikuta kweli ina jina la Brown.
Mmoja wa wazee wa jirani na kina Salma aliongea "ninyi nyote hamjui kitu...bado watoto wadogo huyu mwenzenu anachosema ni kweli kabisa ninyi mnamuona muongo..huyu kijana alikutana na mzimu wa Salma ukamfanyia mazingara hakujua kama ulikuwa mzimu...pole sana kijana wangu" watu wote pale makaburini walipatwa na woga,walianza kutwanyika mmoja baada ya mwingine kila mmoja na njia yake,walijikuta wamebaki wachache wakati lilikuwa kundi kubwa la watu,waliondoka kurudi nyumbani na Brown alirudi kwake.
Akiwa nyumbani hali ya woga ilitanda moyoni mwake alikuwa akisikia hata kijiko kimeanguka alishtuka kama amesikia mlio wa bomu,lakini wakati huo huo akili ilimwambia si kweli alikufa,Salma yupo hai,aliazimia kupeleleza ili ajue ukweli,siku hiyo hakuweza kulala kwa woga wa kutokewa na mzimu wa Salma,ilikuwa yapata saa tano za usiku akiwa kwenye dimbwi la mawazo alishtushwa na mlango kugongwa "nani?" aliuliza Brown lakini hakujibiwa,aliinuka na kuusogelea mlango "nani?" aliuliza kwa mara nyingine tena lakini hakujibiwa,alizidi kupatwa na wasiwasi,mlango uliendelea kugongwa kwa nguvu,alipiga moyo konde na kuamua kuufungua,alipoufungua............ITAENDELEA
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/3cDxP4r
No comments:
Post a Comment