Baba yangu alikuwa tajiri sana, hakuwa akiishi na mama yangu sababu ambayo sijaijua mpaka leo. Nilimpenda sana baba kwa sababu kila alipokua akija kunitembelea kwa mama alikuwa akiniletea zawadi mbalimbali pamoja na pesa.
Ingawa mama yangu alikuwa akinikatisha tamaa kwa kuniambia baba yangu si mtu wa kumuamini hata kidogo. Mimi sikusikiliza! Aliniambia kuwa baba yangu hanipendi kwani kama angekuwa akinipenda angenipeleka kusoma katika shule nzuri zaidi wanazosoma watoto wake wengine tofauti na ile niliyokuwa nikisoma.
Lakini mimi niliendelea kumpenda baba yangu.
Maisha yangu yalibadilika pale mama yangu alivyofariki kwa ugonjwa uliosababisha avimbe miguu yote miwili. Kipindi hicho nilikuwa na miaka 12 tu nikiwa bado shule ya msingi darasa la saba.
Maisha yangu yalibadilika pale mama yangu alivyofariki kwa ugonjwa uliosababisha avimbe miguu yote miwili. Kipindi hicho nilikuwa na miaka 12 tu nikiwa bado shule ya msingi darasa la saba.
Kabla ya kufariki nakumbuka aliniambia kwamba "mwanangu mimi naondoka, lakini kumbuka kuwa matatizo yako ndio yameanza rasmi. Mimi ndio nilikuwa muhimili wako hapa duniani na sasa aliyebakia ni Mungu pekee. Kuwa na imani nae atakusaidia"
Nililia nililia sana kuona mama yangu mpendwa akiniacha. Lakini bado nilikuwa na matumaini na baba yangu ambaye alionekana kunijali.
Baada ya mazishi nilichukuliwa na baba kwenda kuishi kwake. Na kuanzia hapo ndipo nikaanza kupata mateso. Nilikuwa nikifanya kazi zote za nyumbani peke yangu hadi kuwafulia nguo watoto wa mama mwingine waliokuwa na dharau na ambao kimsingi walikuwa wakubwa kuliko mimi. Baada ya kumaliza darasa la saba na kufaulu vizuri kwenda kidato cha kwanza baba aliniambia hana pesa za kuniendeleza.
Hapo ndipo nilipoamini yale mama aliyokua akiniambia. Nililia sana kwa kukosa elimu hasa ukizingatia nilikuwa napenda sana kusoma lakini siku zote nilikuwa nikimuomba Mungu aniondoe na haya majanga kama mama alivyokua akiniambia!
Baada ya miaka 8 ya kukaa tu nyumbani, niliamua niolewe. Nilikuwa na miaka 20 na nilipata boyfriend ambae alikuwa akinipenda sana. Yeye alikuwa na miaka 28. Alikuwa ni kijana mzuri, na mwenye busara. Hakuwa tajiri ila nilijiambia kuwa tunaweza tukatengeneza maisha pamoja.
Lakini baada ya baba kugundua kuhusu uhusiano wetu, alinisakama sana na akamtisha yule kijana kuwa atamuua! Masikini ya Mungu yule kijana alikata tamaa na mimi. Sijui baba alikua na mpango gani na mimi.
Nilimchukia mno baba yangu lakini baadae nikaja kugundua kuwa kila kitu kilikuwa kikipangwa na mama yangu wa kambo ambae watu walikuwa wakiniambia kuwa amemroga baba yangu. Ingawa mimi sikua nina amini sana ushirikina.
Miaka miwili baadae, nilitoroka nyumbani baada ya kuona mustakabari wangu haueleweki. Niliondoka na kwenda kumtafuta mchumba wangu ambae alikuwa mkoa mwingine mbali na nilipokua nikiishi. Nilimpata na alifurahi sana kunipata. Alinichukua na kunipeleka kwao kunitambulisha na tulifunga ndoa ya kimila huko kwao.
Baba alinitafuta sana lakini hakuweza kunipata, ni mpaka pale nilipokua na ujauzito ndipo alipofanikiwa kunipata ilikua ni baada ya miaka mitano! nikaambiwa kuwa baba yangu ni mgonjwa sana. Na alikuwa akinihitaji. Nilienda na kumuona. Aliniambia nimsamehe sana kwa yote aliyonifanyia kwamba ikikuwa ni mipango ya shetani. Nilimsamehe sikuwa na kinyongo nae. Alinipa sehemu ya ardhi yake na pesa kiasi fulani. Na ndipo nilipoamini kuwa kweli alikuwa amerogwa.
Baada ya siku tatu baba yangu nae aliaga dunia. Nililia sana ila sikuwa na cha kufanya zaidi ya kumuombea akapumzike kwa amani!
Niliendelea kuishi na Mume wangu, na baada ya kipindi kirefu cha ugumu wa maisha tuliweza kukuza miradi yetu mbalimbali na kuwa na utajiri mkubwa tu! Na nilishikwa na mshangao pale mama yangu wa kambo alipokuja kunitembelea na kuniomba msamaha huku akiniambia nimlaumu yeye kwa kila magumu yote nikiyopitia.
Sikuwa na kinyongo! Nilimsamehe. Na kwa sasa bado naendelea kuishi na mume wangu. Mungu ametujalia watoto wawili, mvulana na msichana wenye furaha siku zote. Wale ndugu zangu wa mama wa kambo wote bado wako nyumbani na wote wamezalishwa na wanaume wamewakimbia, na mmoja amefariki mwaka jana baada ya kuugua muda mrefu na gonjwa la UKIMWI. Ila kabla ya yote hua namshukuru MUNGU kwa matendo ya ajabu aliyonitendea.
🌏ZINGATIO🌍
Ingawa tunaishi katika maisha yaliyojaa matatizo ya kila aina kama vile, kusalitiwa katika mapenzi, kuanguka kiuchumi, kudharauliwa na kutengwa ambako kwa namna moja kunasababishwa na binadamu wenzetu. ILA MUNGU siku zote yupo kwa ajli yetu na atatufanya tufanikiwe na kuinuliwa ili wanaotudharau waje kutusalimia kwa heshima zote.
Kama una amini kwa uwezo wa MUNGU kwamba atakufanya uendelee kufanikiwa kwanini usiseme AMeenIngawa tunaishi katika maisha yaliyojaa matatizo ya kila aina kama vile, kusalitiwa katika mapenzi, kuanguka kiuchumi, kudharauliwa na kutengwa ambako kwa namna moja kunasababishwa na binadamu wenzetu. ILA MUNGU siku zote yupo kwa ajli yetu na atatufanya tufanikiwe na kuinuliwa ili wanaotudharau waje kutusalimia kwa heshima zote.
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2TEdjtc
No comments:
Post a Comment