Ukiangalia kwenye masuala ya urembo, unaweza kusema wanawake wako katika ulimwengu wao kwa jinsi wanavyojikita kuboresha mionekano yao.
Kutokana na hali hiyo, baadhi yao ambao hawana mionekano mizuri ya asili huonekana kuhangaika katika kutafuta namna ya kujibadilisha ili tu wapendeze na kuwavutia watu hasa wanaume.
Katika Ukurasa wa Facebook wa East Africa Television (EATV) iliwekwa mada ya Funguka iliyouliza kuwa "Unadhani wanaume ndiyo sababu kubwa ya wanawake wengi kubadili mionekano yao?", ambapo wafuatiliaji wengi wametoa mtazamo wao kuhusiana na swali hilo.
Wa kwanza kabisa ni Lema Thomas ambaye amesema, "bila shaka wanaume ndio sababu, Mungu awabariki wanawake wote walioweza kutunza uhalisia wao kwani ndo wenye kupendeza na kuvutia".
Wa pili ni Joyce Mziwanda ambaye amesema "sio kweli, wanawake hujibadili tu kwasababu ya wanawake wenzao maana akiona mdada mwenzie kapendeza tu nae atataka kuwa kama yule, hata mimi nina dada hapa kananiiga kila ninachofanya kimuonekano na yeye anafanya hivyo hivyo ".
Juhudy Mtega anasema wanawake wengi wanajihisi wakiwa weusi hawatapendwa na wanaume, kitu ambacho sio kweli kwani wanaume tunapenda sana uzuri asilia na tabia sio weupe au kujiongeza makalio.
Mchangiaji mwingine, Steven Msigwa amesema "yaani kama mtu ameweza kutoa mimba ili kulinda umbo, atashindwaje kujibadilisha umbo lake kwa ajili yetu, yani serikari inaweka wanasheria kwaajili ya makosa ya jinani na wanawake hao hao ndio wanatoa mimba kulinda maumbo"
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UFUNDI WA MAPENZI BOFYA HAPA KUDOWNLOAD
Sunday, September 1, 2019
Sababu kuu ya wanawake kujichubua
Tags
# Jifunze mapenz
About Sportswidely
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Jifunze mapenz
Labels:
Jifunze mapenz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment