Akamatwa kwa Uharibifu Wa Sanamu Ya George Floyd - Mapenz Wakubwa

Thursday, October 28, 2021

Akamatwa kwa Uharibifu Wa Sanamu Ya George Floyd






Hizi ni ripoti za kutokea New York, Marekani  ambapo mtu mmoja anayejulikana kama Micah Beals mwenye umri wa miaka 37 amekamatwa kwa kosa la kuiharibu sanamu ya marehemu George Floyd iliyowekwa katika eneo la bustani la Union Square.

 

Katika vipande vya video vilivyosambaa mitandaoni, vinamuonesha jamaa huyo akirusha rangi ya kijivu kuelekea kwenye sanamu hiyo mapema mwezi huu, polisi walitangaza ofa ya dola 3,5000  zaidi ya shilingi  milioni 7  kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu aliyetekeleza kitendo hico cha kuiharibu sanamu hiyo.

 

Floyd aliuawa na Polisi wa Minneapolis May 2020 na kupelekea maandamano makubwa nchini Marekani, uharibifu wa sanamu hiyo unahusianishwa na muendelezo wa ubaguzi wa rangi uliopo nchini humo.

Cc; @bakarimahundu


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3mkRvRn
via IFTTT

from mapenzi kitandani https://ift.tt/2XREO7h

No comments:

Post a Comment