Dar es Salaam. Wanasiasa, wananchi na viongozi wa dini wamemshukia Mbunge wa Kawe(CCM) ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima juu ya kauli yake kuwa daktari atakaye ‘shadadia’ suala la chanjo bila kufanya utafiti wa kina kujua madhara ya muda mrefu na mfupi atakufa.
Askofu Gwajima aliyasema hayo katika ibada ya Jumapili wakati akiwahubiria waumini wake huku akionyesha mashaka kuwa chanjo za Uingereza na Tanzania zinaweza kuwa hazina content sawa.
Kauli ya Askofu Gwajima imekuja ikiwa ni siku moja tangu Serikali ipokee msaada wa dozi 1,058,400 za chanjo ya corona zilizotolewa na nchi ya Marekani kupitia mpango wa Covax facility.
“Mmefanya uchambuzi wa kina kujua chemical content ya hiyo chanjo ni nini, mimi namtaka daktari atakayeshadadia nitakula naye meza moja utakufa daktari, utakufa utaona.”
Kufuatia maneno yake watu mbalimbali wametoa maoni yao kupitia kipande chake cha video kinachosambaa mitandaoni huku wengi wao wakionekana kukemea kauli hiyo.
Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika “Kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo na dhamira ya Serikali kuleta chanjo nchini haikubaliki. Ni hatari kupotosha watu wanaotuamini kuhusu mambo ambayo hatuna utaalam nayo,”
“Mjadala kuhusu usalama wa chanjo ni sahihi lakini kiapo kwamba Serikali imeileta kuwadhuru watu si sahihi.” aliandika
Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania (CCT), Dk Fredrick Shoo amehimiza wananchi kuendelea kujikinga na wimbi la tatu la corona na kusisitiza kuendelea na maombi ya kufunga na kutubu, ili kujinusuru na janga hilo.
“Nawaonya viongozi wa dini kuacha kuhusisha suala la chanjo ya Covid 19 na mpango wa shetani kwani huko ni kumjaribu Mungu,” alisema.
Solomon Franco @mamgunda1 kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika “Huyu hana elimu ya utabibu lakini ndio anaongoza kupotosha watu,”
Aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliiomba Serikali imchukulie hatua Askofu Gwajima kwa sababu atasababisha watanzania wengi wafe kwa mafundisho yanayopotosha
“Hana scientific evidence kwa vitu anavyozungumza, hajui mambo ya kitatibu na siyo mtabibu, ningemshauri na nimsihi aheshimu taaluma za watu, akawasikiliza wataaluma,”
“Pia kitendo cha kusema wanaopigia chapuo madawa haya wamepewa pesa anamaanisha anamtuhumu hata Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama chake, hivyo ni vyema achukuliwe hatua,” alisema.
Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu na maadili ya chama.
Taarifa iliyotolewa leo na CCM, Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka inawakikishia wanachama na Watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi iyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM
from Udaku Special https://ift.tt/3y8wnS7
via IFTTT
from mapenzi kitandani https://ift.tt/3kWMGgS
No comments:
Post a Comment